HIZI HAPA NI DALILI ZA USONJI
1.Tatizo la kuchangamana na jamii
👉Anakuwa na changamoto wakati wa kutengeneza marafiki
👉Anakuwa na changamoto kwenye kushiriki furaha au mafanikio yake.
👉Mtoto anakuwa anajitenga na wengine na kupendelea kukaa pekee yake
· 👉kukwepesha macho wakati anapokuwa anaangaliana
na wengine au akiangaliwa.
2.Tatizo katika mawasiliano
👉Kushindwa kuongea ingali umri wa kuongea umefika
👉Changamoto kwenye kuanzisha na kuhimili au kuendeleza mazungumzo
👉Kurudia maneno unayo mwambia anakuwa hana uwezo wa kujibu zaidi ya kurudia unachomwambia
3. Tabia za kijirudiarudia
· 👉 Hii huhusisha mtoto kuwa na tabia za kujiumiza
kama vile kujipigiza kwenye vitu,kubamiza vitu kama mlango,kupanda sehemu za
juu akitaka kujirusha.
· 👉 kupenda kutembeatembea,
· 👉kufunika masikio kwenye sauti kubwa na wengine
kupendelea sauti kubwa
· 👉kufumba macho kwenye mwanga mkali
· 👉kukataa mabadiliko ya vitu mfano chakula ,sehemu ya kulala, eneo jipya tofauti na alilolizoea
· 👉kucheka bila sababu hata kama wengine hawaoni
sababu za kucheka
Ukiona dalili hizi anazo mwanao, mtoto wa rafiki,ndugu yako basi tupigie kwa namba zifuatazo;
Ndamo Rehabilitation Solutions Center
Mwanza Dispensary,Mecco Kusini-Majanini
Phone:0748199113/0629199113
Email: daniellysamweli88@gmail.com

Maoni
Chapisha Maoni