JE UNAJUA NINI MAANA,VISABABISHI NA DALILI ZA SONONA?
Kiukweli hili limekuwa ni tatizo kubwa sana katika jamii ndio maana tumekuwa tukishuhudia majanga makubwa sana kama watu kujiua kwa vifo vya aibu kama kujinyonga watu kushindwa kuhimili mikiki ya maisha ya kila siku.
SONONA ni tatizo la afya ya akili
linalojitokeza kwa hisia za huzuni, kukata tamaa, na kupoteza hamu au furaha
katika shughuli za kila siku. Tatizo hili linawezaleta athari katika mawazo,
hisia, tabia, na ustawi kwa ujumla. Hapa kuna maelezo kuhusu chanzo na dalili.
Chanzo cha SONONA:
👉Sababu za Kibaolojia: Kutokuwa sawa kwa
kemikali za ubongo (neurotransmita) kama vile serotonini, norepinephrine, na
dopamine kunaweza kuchangia sonona.lakni pia sababu za kurithi zinaweza
kupelekea mtu kupata kisonona.
👉Mambo ya Kisaikolojia: Tabia fulani za
kibinafsi, kutokujiamini, historia ya matukio au unyanyasaji, na upungufu wa
ujuzi wa kukabiliana na matatizo kunaweza kuwafanya watu kuwa hatarini zaidi.
👉Sababu za Kimazingira: Mabadiliko
makubwa katika maisha, kama kupoteza mtu wa karibu, matatizo ya kifedha,
matatizo ya mahusiano, au msongo wa muda mrefu, yanaweza kusababisha sonona.
👉Matatizo ya kiafya: matatizo ya kiafya kama
maumivu ya muda mrefu, matatizo ya tezi, kutokuwa sawa kwa homoni, au historia
ya magonjwa mengine ya afya ya akili, zinaweza kuongeza hatari ya sonona.
je, umekuwa na dalili kama hizi tajwa hapo chini?
👉Huzuni kwa muda murefu,kujisikia huna
thamani, au kukata tamaa.
👉Kupoteza hamu au furaha katika shughuli
ambazo hapo awali ulizipenda yaani kushuka kwa ufanisi kazini.
👉Mabadiliko katika hamu ya kula na uzito
(kuongezeka au kupungua) hii kutofautiana kutoka mtu mpaka mtu kwani wengine hupelekea kukosa hamu ya chakula na wengine kula kupita kiasi.
👉Kupata shida kulala (kutokuwa na
usingizi au kulala sana).
👉Uchovu na motisha kupungua.
👉Kupata shida katika kuzingatia, kufanya
maamuzi, au kukumbuka mambo.
👉Hisia za kutokuwa na thamani, hatia, au kujilaumu.
👉Mawazo ya mara kwa mara juu ya kifo au
kujiua.
👉kuwa na hali ya kusahau mara kwa mara
👉Dalili za mwili kama vile maumivu ya
kichwa, maumivu ya tumbo, au maumivu ya muda mrefu.
itaendelea kuhusu matibabu yake
Ushauri
Tatizo hili linasuluhisho ukihisi una
baadhi ya hizo dalili tajwa hapo juu tafuta msaada wa wataalamu haraka sana
kabla hujafikia hatua mbaya za kujiua na athari zingine
Kwa msaada wasiliana na Ndamo Rehabilitation Solutions
Call us on +255748199113
whatsap us on +255629199113
Tunapatikana: Mwanza-Mecco Majanini

Maoni
Chapisha Maoni